Yanga yatangaza hali ya hatari

Muktasari:

Mabingwa hao watetezi wameshinda kwa mara ya kwanza mabao matano msimu huu

Dar es Salaam. Kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajingwa 'Fusso' amesema wakati wanaanza ligi walikuwa hawatengenezi nafasi nyingi za kufunga lakini sasa mambo yamejipa.

“Tulifanyia kazi suala la kutokutengeneza nafasi na tukalimaliza likajitokeza tatizo lingine la washambuliaji wetu kutokufunga na kukosa nafasi nyingi za wazi.

“ Tuliwapa mbinu za kuweza kutumia nafasi hizo na kuanza mechi hii ya Mbeya City wameweza kufanya yale ambayo tunahitaji kutoka kwao,” alisema Nsajigwa ambaye alistaafu Yanga kwa heshima.

Mchezaji huyo aliyewahi kung'ara na Prisons na Moro United aliongeza kuwa; “Mwanzoni timu ilikuwa haipati ushindi wa mabao mengi lakini kwa sasa kikosi chetu kinaanza kufunguka na kupata ushindi mzuri ni matarajio yetu tutaendelea hivi hivi kwa sababu lengo letu ni kutetea ubingwa msimu huu.”