Liverpool yatupiwa Man United, Barca kwa Spurs

Muktasari:

Mashindano hayo ni kwa ajili ya kujipima nguvu kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi mbalimbali

London, England. Manchester United wataivaa Liverpool Julai 28 katika mchezo wa mashindano ya International Champions Cup.

Mechi hiyo itachezwa wiki mbili baada ya kumalizika kwa Kombe la Dunia, Russia kwa  watani hao wa jadi kuonyeshana kazi katika mashindano hayo yanayofanyika Marekani kwenye Uwanja wa Big House, Michigan.

Pia kuna timu nyingine mbili za England zitakazocheza katika mashindano hayo.

Manchester City na Tottenham wenye wachuana katika mashindano hayo yanayozikutanisha timu kubwa za Ulaya.

Mashindano hayo yamepangwa kuanza Julia 20, ikiwa ni siku sita baada ya mchezo wa fainali Kombe la Dunia.

Vijana wa Pep Guardiola watacheza mechi ya kwanza dhidi ya Borussia Dortmund mjini Chicago katika siku ya ufunguzi.

Siku mbili baadaye Liverpool itawajaribu Wajerumani hao katika uwanja huo.

Man United mechi ya kwanza watacheza Julai 25, dhidi ya AC Milan mechi itakayofanyika Pasadena.

Pia, katika siku hiyo Manchester City watakuwa na kibarua na wabaya wao Liverpool, huku Spurs itacheza dhidi ya Roma, Dortmund itacheza tena na Roma, wakati Juventus watajiuliza kwa Bayern Munich.

Katika siku ambayo Man United itaivaa Liverpool, Julai 28, Man City wanaokaribia kupata ubingwa wa England wataonyeshana kazi na miamba ya Ujerumani,Bayern Munich jijini Miami.

Mjini Pasadena, Tottenham wataonyeshana kazi na Barcelona wakati Benfica wataivaa Juventus kwenye Uwanja wa Red Bull Arena, New York.

Julai 31, Man United watarejea uwanja kumkabili kijana wao Cristiano Ronaldo na

Real Madrid jijini Miami. Katika siku hiyo Spurs watafunga kwa kucheza AC Milan mjini Minneapolis.