Kombe la Chalenji kuchezwa Desemba

Muktasari:

Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye aliimbia BBC Sport kuwa mashindano hayo yatafanyika Desemba.

Nairobi, Kenya. Baraza la Mashirikisho ya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) limethibisha kufanyika kwa mashindano ya Chalenji mwaka huu baada ya kushindwa kuchezwa mwaka jana.

Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye aliimbia BBC Sport kuwa mashindano hayo yatafanyika Desemba.

"Siwezi kusema ni nchi gani itakuwa mwenyeji kwa sababu bado mazungumza yanaendelea," alisema Musonye

Pia, alithibisha kufanyika kwa mashindano ya vijana ikiwa ni ishara ya kuchezwa kwa mashindano ya Chalenji.

"Pia, kutafanyika mashindano ya Cecafa U-17, yatakayofanyika Burundi kuanzia Oktoba na kufuatiwa na Kombe la Chalenji," alisema kwa kujiamini Musonye.

Uganda Cranes ndiyo mabingwa watetezi wa Kombe la Chalenji baada ya kuifunga Rwanda katika fainali zilizofanyika Ethiopia mwaka 2015.

Cecafa unaundwa na nchi wanachama 12 ambao ni; Uganda, Sudan, South Sudan, Eritrea, Somalia, Ethiopia, Kenya, Tanzania, Rwanda, Burundi, Djibouti na Zanzibar.