Kombe Bandia la Simba lanufaisha wajanja

Muktasari:

Baadhi ya wapiga picha, wamekuja na kombe bandia uwanjani hapo na kuliweka kwenye moja ya mabango ya klabu hiyo lililopo nje ya jukwaa la kijani na kuwatoza fedha mashabiki mbalimbali wanaopiga picha na kombe hilo bandia.

Wakati Simba ikiwa haijaweka utaratibu wa mashabiki kupiga picha na Kombe kwenye tamasha Simba Day, baadhi ya watu wametumia nafasi hiyo kuvuna pesa bila jasho.

Baadhi ya wapiga picha, wamekuja na kombe bandia uwanjani hapo na kuliweka kwenye moja ya mabango ya klabu hiyo lililopo nje ya jukwaa la kijani na kuwatoza fedha mashabiki mbalimbali wanaopiga picha na kombe hilo bandia.

Kila shabiki anayepiga picha na Kombe hilo Bandia amekuwa akitozwa kiasi cha Shilingi 1000 ambazo zinaishia kwa wapiga picha hao ambao wamekuwa wakizisafisha hapo hapo na mtambo uliopo pembeni.

Mbali na hilo, nje ya uwanja wa Taifa kumekuwa na kundi kubwa la wafanyabiashara wanaouza jezi na skafu feki zenye nembo ya klabu hiyo lakini hakuna hatua zozote wanazochukuliwa huku vikiendelewa kununuliwa kwa wingi na mashabiki wa Simba.

Hivi karibuni Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alisema klabu hiyo imejipanga kuanza kuwashughulikia wafanyabiashara ambao wamekuwa wakitumia nembo ya Simba kutengeneza na kuuza bidhaa feki