Kocha Valverde atoa ya moyoni sakata la Neymar

Muktasari:

  • Paris St-Germain imeripitiwa kutangaza kufikia dau la Pauni 199 milioni ili kumsajili mchezaji huyo.

Kocha wa Barcelona, Ernesto Valverde ameibuka na kusema kwamba matamanio yake ni kuona Neymar anaendelea kuitumikia Barcelona.

Paris St-Germain imeripitiwa kutangaza kufikia dau la Pauni 199 milioni ili kumsajili mchezaji huyo.

Licha ya Rais wa Barcelona, Josep Bartomeu kuieleza BBC Sport kuwa mchezaji huyo hauzwi lakini dau la PSG huenda likatibua kila kitu.

Ververde baada ya mechi ya Juventus na Barcelona iliyoisha kwa Neymar kutupia mabao 2-1, alisisitiza kuwa wanatambua thamani ya mchezaji huyo anapokuwa uwanjani hivyo watatumia kila mbinu kumbakisha.