Sherehe za ubingwa zamsababishia makubwa kocha Simba

Muktasari:

Lechantre alikasirishwa na kitendo cha kumaliza mchezo huo huku wakiwa wamefungwa na Kagera Sugar bao 1-0 na kuharibu rekodi ya kutokufungwa ndani ya mechi 28 walizocheza.

Dar es Salaam: Katika hafla ambayo Simba walikabiziwa kombe lao la Ligi Kuu Bara na Rais John Magufuli hakuna mtu aliyetoka uwanjani hapo akiwa amechukizwa kama kocha wao mkuu, Mfaransa Pierre Lechantre.

Lechantre alikasirishwa na kitendo cha kumaliza mchezo huo huku wakiwa wamefungwa na Kagera Sugar bao 1-0 na kuharibu rekodi ya kutokufungwa ndani ya mechi 28 walizocheza.

Kwani licha ya kuwepo burudani tofauti zilizokuwa zinaendelea uwanjani hapo, Lechantre alikuwa kama mtu aliyelazimishwa kusheherekea hadi wachezaji walimpomfuata na kumbeba juu.

Lechantre amesema: "Siwezi kuwa na furaha wakati lengo letu lilikuwa ni kushinda mechi zetu zote zilizo mbele yetu bila kujali tuko nafasi gani, pia ilikuwa siku muhimu na ndiyo tumefungwa."

Katika hafla hiyo ambayo kwao ilikuwa ni historia kubwa kwa Simba na ligi kuu kwani ni mara yao ya kwanza tangu klabu hiyo ianzishwe mwaka 1935 ikiitwa jina la Sunderland.

Simba imebakiza mchezo mmoja wa ligi kuu ili kukamirisha ratiba ya michezo yao 30 ambapo watasafiri kwenda Songea kucheza na Majimaji FC.