Kocha Mayanga ateremsha kikosi cha wachezaji 21

Muktasari:

Makipa ni Aishi Manula (Simba), Ramadhani Kabwili (Yanga) na Peter Manyika (Lipuli

Dar es Salaam. Wachezaji 21 wameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars na kocha wa timu hiy, Salum Mayanga kwa ajili ya mchezo wa kirafiki utakao chezwa Oktoba 7 dhidi ya Malawi.
Makipa ni Aishi Manula (Simba), Ramadhani Kabwili (Yanga) na Peter Manyika (Lipuli).
Walinzi ni Gadiel Michael (Yanga), Erasto Nyoni (Simba), Boniface Maganga (Mbao FC), Adeyuni Saleh (Kagera Sugar), Abdi Banda (Baroka FC), Kelvin Yondani (Yanga) na  Salim Mbonde (Simba).
Viungo ni Himid Mao (Azam), Hamis Abdallah (Sonny Sugar), Mzamiru Yassin (Simba), Raphael Daud (Yanga),Simon Msuva (Difaâ El Jadidi), Shiza Kichuya (Simba), Orgenes Mollel (FC Famalicão), Abdul Hilal (Tucker FC) na Ibrahim Ajib (Yanga).
Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk) na Mbaraka Yusuph (Azam).