Kocha Lipuli FC atoa onyo mechi zinazofuata

Muktasari:

  • Katika mchezo wa jana uliofanyika katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora, Lipuli ilipata goli pekee dakika ya 78 kupitia kwa mshambuliaji wake Lambeli Jerome.

Baada ya Lipuli FC kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stand United ya Shinyanga, Kocha Mkuu wa Lipuli FC, Selemani Matola ametamba kuwa timu yake itaendeleza dozi kwa timu itakazokutana nazo.

Katika mchezo wa jana uliofanyika katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora, Lipuli ilipata goli pekee dakika ya 78 kupitia kwa mshambuliaji wake Lambeli Jerome.

“Timu zote zilicheza vizuri lakini vijana wangu niliwapa maelekezo na wameyafuata. Nimepata ushindi, hizi ni salamu kwa timu tutakazokutana nazo tutaendeleza dozi," alisema Matola.