Kocha Conte achukua mbinu za Jose Mourinho uwanjani

Friday August 11 2017

 

England. Maisha kila siku yanabadilika, ndivyo unavyoweza kuielezea kwa kocha Antonio Conte ambaye hivi sasa ameamua kuiga mtindo wa Kocha Jose Mourinho anapohimiza kikosi chake uwanjani kwa vitendo.

Conte alionekana katika mechi kadhaa za hivi karibuni akitumia lugha za ishara na kuutumia mwili wake vilivyo anaposisitiza jambo kwa mchezaji uwanjani.

Mechi ya Jumapili iliyopita ya Ngao ya Jamii iliyowakutanaisha Chelsea na Arsenal England, kocha huyo hakuwa anatulia uwanjani na kila alipotoa maelekezo alikuwa akisisitiza kwa kutumia ishara ya mikono.