Kocha Asante Kototo azitolea macho Simba, Yanga

Muktasari:

  • Amesema, anajua Tanzania kuna timu kubwa zenye ushindani kama Simba na Yanga hivyo anatamani kuja kufanyanya kazi hapa.

Dar es Salaam. BONGO raha bwana kwani Kocha Mkuu wa Asante Kotoko ya Ghana, Samuel Kwasi ametamka kuwa anatamani kuja kufanya kazi na moja ya klabu nchini kutokana na kuvutiwa na mazingira ya Tanzania.

Amesema, anajua Tanzania kuna timu kubwa zenye ushindani kama Simba na Yanga hivyo anatamani kuja kufanyanya kazi hapa.

Kocha huyo ambaye ni Mghana alikuja nchini pamoja na kikosi hicho, wakacheza mechi ya kirafiki na Simba katika sherehe za Simba Day.

Amesema: "Kilichonivutia ni namna ambavyo Watanzania walivyokuwa na hamasa kwenye soka kama namna nilivyoona, nimependa na natamani sana kuja kufanya kazi hapa."

Amesema, hiyo ndiyo hamu yake kubwa na amejikuta akipenda baada ya kufika nchini.      

Katika mchezo huo uliopigwa siku ya Simba Day matokeo yalikuwa ni sare ya bao 1-1.