Kipa wa Arsenal atua Juventus kurithi mikoba ya Buffon

Muktasari:

Kipa huyo anakwenda Juventus ambako kuna kipa mahiri namba moja Gianluigi Buffon ambaye hivi karibuni kulikuwa na taarifa kuwa mkataba wake unaelekea kuisha, hivyo alipendekeza kutafutwa mapema mbadala wake.

London, England. Kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny amesajiliwa Juventus kwa dau la Pauni 10 milioni baada ya kutumika kwa miaka miwili katika klabu ya Roma alikotolewa kwa mkopo.

Kipa huyo anakwenda Juventus ambako kuna kipa mahiri namba moja Gianluigi Buffon ambaye hivi karibuni kulikuwa na taarifa kuwa mkataba wake unaelekea kuisha, hivyo alipendekeza kutafutwa mapema mbadala wake.

Mchezaji huyo ataanza maisha mapya klabuni hapo ambako amesajiliwa kwa miaka minne na mabingwa hao wa Italia.

Raia huyo wa Poland mwenye miaka 27 amecheza mechi 38 akiwa Roma msimu ulioisha na kufanikiwa kupangua hatari nyingi jambo lililomfanya kiwango chake kuonekana.

Mchezaji huyo alicheza mechi 132 alipokuwa Arsenal ambako aliitumikia kwa miaka minane.