Kenya yanyakua medali 14 Mashindano ya Riadha ya Vijana ya Dunia

Friday July 21 2017

 

Kenya. Mashindano ya Riadha ya Vijana ya Dunia yamehitimishwa leo nchini Kenya, huku Taifa hilo likishika nafasi ya nne kwa jumla baada ya kunyakua medali 14.

Mashindano hayo yalianza kutimua vumbi tangu Jumatano tarehe 12 na kufikia tamati leo Jumapili.

Mashindano hayo yalihusisha wanariadha takribani 800 kutoka mataifa 131 nchi wanachama wa Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF).

Mshindi wa kwanza wa jumla kwenye kunyakua medali ilikuwa ni Afrika Kusini, wa pili China wa tatu Cuba.

Mashindano hayo yaliwahi kufanyika pia Morocco mwaka 2005 na mwaka huu itakuwa mara ya mwisho kuandaliwa na IAAF.