Karume Boys yawekwa hadharani

Zanzibar. Wachezaji 20 wamechaguliwa kuunda timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Karuma Boys’ itayoshiriki mashindano ya Cecafa nchini Burundi.

Kocha wa timu hiyo, Mzee Ali abdallah alisema wachezaji hao wamepatikana baada ya kufanya mchujo uliojumuisha vijana 47.

Wachezaji hao ni makipa: Dotto Shauri kutoka (Black Sailors),Yakubu Ali (Real Kids), Mabeki: Shabani Pandu (Villa United), Mohammed Ibrahim (Villa United), Mohammed Jeilan (Miembeni City), Omari Haji (Mlandege), Selemani Salum (Kaskazini ), Nudrin Vuai (Mwambao) na Abubakar Silima (Z.F.D.C).

Viungo: Abdulrahman Juma (KMKM), Eliyasa Juma (Taifa ya Jang’ombe), Ibrahimu Ali (Villa), Haji Suleiman (JKU), Abubakar Khamis (Mafunzo), Masoud Mohamed (Spider), Suleiman Nassor (Dogo Moro) na Mundhir Imani  (Chipukizi).

Washambuliaji: Ibrahim Yahya (Black Sailor), Abdillah Issa (Dogo Moro), Abdulhamid Juma (Mlandege) na Nassor Fasihi wa Mapembeani.