Jose Mourinho afuta mpango wa kumhamisha Ronaldo

Friday July 21 2017

 

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amefuta rasmi mpango wa kumsajili msahambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.

Mourinho alisema kwa sasa hana mpango tena wa kumsajili mchezaji huyo kwa sababu klabu hiyo haiwezi kumuuza mchezaji wa aina ya Ronaldo katika kipindi hiki.

Ronaldo alinunuliwa na Real Madrid mwaka 2009 kwa uhamisho wa Pauni 80 milioni akitokea Manchester United lakini imekuwa ngoma nzito kutaka kumridisha.

Awali, uongozi wa klabu hiyo ulitaka dau la Pauni 135 milioni kwa klabu inayomhitaji na baadaye wakafuta mpango wa kumuuza.