VIDEO: Jezi ya Okwi yapanda thamani Mwanza

Muktasari:

Mfanyabiashara Said Hassan anayejishughulisha na uuzaji wa jezi jijini Mwanza, alisema kuwa jezi ya Okwi imekuwa na wateja wengi kuliko nyingine ikifuatiwa ya Haruna Niyonzima.

Mwanza. Jezi ya mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi inauzika zaidi kuliko za wachezaji wengine hapa jijini Mwanza ikiwa ni kuelekea mechi ya Simba na Mbao FC.
Mfanyabiashara Said Hassan anayejishughulisha na uuzaji wa jezi jijini Mwanza, alisema kuwa jezi ya Okwi imekuwa na wateja wengi kuliko nyingine ikifuatiwa ya Haruna Niyonzima.
"Kwa sasa jezi ya Okwi inauzika sana kuliko nyingine na mashabiki wengi wanasema kuwa huyo ndiye mchezaji anayeibeba timu, nyingine kidogo ni ya Niyonzima," amesema Hassan.