Iniesta achomoka Barcelona

Mchezaji wa Barcelona, Andres Iniesta anaondoka Barcelona katika msimu huu wa kiangazi baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka 22.

Iniesta amekuwa akihusisha kwenda kucheza Ligi Kuu ya China, lakini kwa sasa ameonekana akikaribia kutua klabu ya Vissek Kobe ya Japan.

Vyombo vya habari vimeripoti kwamba nyota huyo anakwenda kutua klabu ya Vissel Kobe ambayo inamilikiwa na mmoja wapo wa wadhamini wa Barcelona, Hiroshi Mikitani

Nyota hyo aliweka picha kwenye mtandao ikimuonyesha akiwa na mmiliki huyo kwenye ndege.

Iniesta aliandika pia kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba sasa anakwenda kwenye makazi mapya huku akiweka alama ya bendera ya Japan na akiwa kwenye ndege.