Mo Ibrahim awaahidi mashabiki Simba

Muktasari:

“Katika nafasi ninazoweza kucheza, mastaa waliopo wana viwango vya juu, ndiyo maana anayekuwa juu ya mwingine ndiye anayetumiwa na kocha huku anayesugua benchi akiumiza kichwa afanye nini ili acheze, hii ni nzuri kumfanya mchezaji asibweteke,” alisema.

KIUNGO wa Simba, Ibrahim Mohammed ‘Mo’ amezungumzia changamoto ya namba anayokumbana nayo ndani ya kikosi hicho.

“Katika nafasi ninazoweza kucheza, mastaa waliopo wana viwango vya juu, ndiyo maana anayekuwa juu ya mwingine ndiye anayetumiwa na kocha huku anayesugua benchi akiumiza kichwa afanye nini ili acheze, hii ni nzuri kumfanya mchezaji asibweteke,” alisema.

“Ushindani ni kitu kizuri, unafanya timu iwe mwiba kwa wapinzani na kutimiza malengo, mfano mzuri Simba tunataka ubingwa ambao mashabiki wetu wameungoja ndani ya miaka minne, binafsi naamini bado nina nafasi kubwa ila napambana.”

Simba juzi Jumapili ilicheza na Mtibwa Sugar na kutoka sare ya bao 1-1, mashabiki walikuwa wakiulizana kilichompata Mo hadi asionekane katika mechi hiyo. Amewajibu alikuwa na matatizo ya kifamilia.

“Najiunga na mazoezi kuelekea mchezo dhidi ya Njombe Mji ambao una ushindani wa aina yake, mashabiki wajue bado nipo,” alisema