Fifa yazichimba mkwara Nigeria, Ghana

Muktasari:

  • Fifa imesema Shirikisho la soka la Nigeria (NFF), linatakiwa kuwarejesha viongozi wa kuchaguliwa kufikia Jumatatu ijayo kinyume cha hivyo nchi hiyo itafungiwa.

Zurich, Uswisi. Shirikisho la soka la kkimataifa (Fifa), limezipa Nigeria na Ghana, tarahe ya mwisho kuamua kama ziko radhi kuadhibiwa ama zinataka kujiepusha na adhabu.

Fifa imesema Shirikisho la soka la Nigeria (NFF), linatakiwa kuwarejesha viongozi wa kuchaguliwa kufikia Jumatatu ijayo kinyume cha hivyo nchi hiyo itafungiwa.

Katika kadhia hiyo ni kuwa Rais wa kuchaguliwa wa NFF, Amaju Pinnick, aling’olewa madarakani wakati akihudhuria fainali za Kombe la Dunia 2018, ambapo kundi la watu walioenda Mahakamani walipewa mamlaka na chombo hicho cha sharia kukaa madarakani.

Ingawa NFF ilitangaza kuwa wahuni hao walitimuliwa kutoka madarakani baada ya fainali za Kombe la Dunia kumalizika lakini ukweli ni kuwa hadi sasa Pinnick bado hajarejehswa madarakani.

Iwapo itafungiwa Nigeria itashindwa kushiriki katika mechi za kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2019 zinazotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwezi ujao.

Kwa upande wao Ghana wamepewa hadi Agosti 27 Serikali kukiachia Chama cha soka (GFA), kuendesha mambo yake na kuiondoa kamati ya usimamizi iliyowekwa na serikali.

Katika taarifa hiyo, Fifa imesema kanuni za Shirikisho hilo inazuia mambo ya soka kuingiliwa na serikali.

Rais wa GFA na mjumbe wa Fifa, Kwesi Nyantakyi alipatikana na hatia ya kuomba na kupokea rushwa kiasi cha dola 65,000 za Marekani kutoka kwa mwandishi wa habari ambazo inaaminika zilikuwa za rushwa.