Dogo Janja apagawisha Copa Umisseta

Muktasari:

  • Dogo janja alikonga nyonyo za maelfu ya mashabiki waliojitokeza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba katika hafla ya ufunguzi wa mashindano hayo uliofanywa na Waziri mkuu, Kassim Majaliwa.

Mwanza. Mwanamuzi Dogo Janja mjanja kweli kweli, leo (Juni 9) ameibukia katika mashindano ya Copa Coca Cola Umisseta na kufanya shoo live iliyowapagawisha wanafunzi wanaoshiriki mashindano hayo.
Dogo janja alikonga nyonyo za maelfu ya mashabiki waliojitokeza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba katika hafla ya ufunguzi wa mashindano hayo uliofanywa na Waziri mkuu, Kassim Majaliwa.
Dogo janja aliimba nyimbo mbalimbali huku akishangiliwa kwa nguvu na wimbo wake ulioshangiliwa zaidi ni ule wa Heelaa aliomshirikisha Madee.