Dilunga: Nimetua Mtibwa mtanikoma

Dar es Salaam. Kiungo wa JKT Ruvu, Hassan Dilunga amejiunga na Mtibwa Sugar kwa mkataba wa miaka miwili.

Dilunga aliyewahi kutamba na Ruvu Shooting, Yanga amesema Mtibwa hawajakosema kumsajili na hawatajua uamuzi huo.

Dilunga alisema Mtibwa itamfanya aonekane upya katika kiwango chake watu walichozoea kumuona nacho, na kutokana na klabu hiyo kuwa na wachezaji wazuri basi kutamfanya aongezeke uwezo kadri siku zinavyozidi kwenda.

“Nina imani nikimiwa hapa Mtibwa nitakuwa bora zaidi ya miaka ya nyuma kutokana na jinsi ambavyo timu hii ilivyo na aina yake ya uchezaji, kwahiyo ni wakati sahihi kwangu mimi kujiunga na hii timu,” alisema Dilunga.