Daniel Sturridge amshangaza Klopp

Muktasari:

Mechi ya Liverpool na PSG ni mwendelezo wa mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya (Uefa) kwa Kundi C.

London, England. Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, amemfagilia mshambuliaji wake Daniel Sturridge, akisema tangu amemfahamu hajawahi kumwona

akicheza kwa kiwango cha juu kama alivyofanya juzi dhidi ya PSG ya Ufaransa.

Liverpool iliikaribisha PSG na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2, Sturridge ndiye aliifungia timu yake bao la kuongoza dakika ya 30 na James Milner akaongeza la pili dakika ya 36 kabla ya mtokea

benchi Roberto Firmino kuipa ushindi dakika ya 90.

Klopp alisema, PSG iliwawekea ulinzi wa kutosha Sadio Mane na Mohammed Salah na kuwapuuza wengine akiwemo Sturridge

aliyewadhibu kabla Firmino, aliyeingia badala yake kuihakikishia Liverpool ushindi.

“Sturridge amecheza mchezo huu katika kiwango cha juu sana

ambacho sijapata kumuona nacho, alikuwa akijiamini na alifanya maamuzi sahihi muda wote,” alisema Klopp.