Dada wa Diamond ashindwa kuvumilia

Muktasari:

Inadaiwa Esma alikamatwa katika msako maalumu wa watu wanaotumia na kuuza bidhaa feki ikiwemo vipodozi na mwandishi  alipopata habari hizo, alifunga safari hadi katika kituo hicho cha polisi na alipofika aliambiwa hakuna kesi kama hiyo, labda aende kituo cha Polisi Central.

Dar es Salaam: Dada wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnums, Esma, anayedaiwa kukamatwa na kupelekwa Kituo Cha Polisi Osyter Bay kwa kosa la kuuza vipodozi feki dukani kwake Sinza Afrika Sana, ameshitushwa na taarifa hizo.

Inadaiwa Esma alikamatwa katika msako maalumu wa watu wanaotumia na kuuza bidhaa feki ikiwemo vipodozi na mwandishi  alipopata habari hizo, alifunga safari hadi katika kituo hicho cha polisi na alipofika aliambiwa hakuna kesi kama hiyo, labda aende kituo cha Polisi Central.

Mwandishi hakuishia hapo, akaenda hadi Polisi Central na alipofika aliambiwa msemaji wa taarifa hizo hayupo, hivyo arudi siku ya pili (leo Jumatatu) atamkuta.

Lakini kwa bahati nzuri Mwandishi alifanikiwa kumpata, Esma jana Jumapili wakati wa  uzinduzi wa kipindi kipya cha 'Nyumba ya Imani' kitakachorushwa Wasafi TV ambayo Mkurugenzi wake ni Abdul Naseeb 'Diamond' ambaye ni kaka wa muhusika huyo.

Ndipo Esma akazungumza na MCL Digital na kufunguka kila kitu: "Mimi sijapelekwa huko polisi, ila nashangaa tu napigiwa simu na  watu wengi wananiuliza umeshatoka? Upo kituo gani? "

"Kiukweli nilivyokuja kusikia eti inshu yenyewe naambiwa nimekamatwa nauza vipodozi feki, nilishangaa sana na nikajua ni mbinu tu ya kutaka kuniharibia biashara na sijui habari hizo zimetokea wapi,"alihoji Esma.