Country Boy: Sitosahau haya maishani

Thursday September 7 2017

 

By FRANK NGOBILE

Dar es Salaam. Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Country Boy amesema hawezi kusahau mambo mawili aliyofanyiwa na mashabiki zake.

Akizungumza na MCL Digital, Country Boy alisema anakumbuka kitendo alichofanyiwa na mashabiki wanawake baada ya kutumbuiza jukwaani.

“Sitosahau ilikua Mbeya nimeshuka kwenye steji alikuja dada mmoja alikuwa akilia kabisa anataka kupiga nami picha alafu anasema alikua na zawadi yangu kabisa kaandika jina langu pale juu Country Boy kiukweli nilifurahi sana na nilipiga naye picha akanipa ile zawadi.”

“Wakati narudi sasa kufungua zawadi hiyo nikakuta kaniwekea nguo yake ya ndani, nilistuka alafu nilicheka sana pia sababu sikujua alikuwa na lengo gani hasa na zawadi kama hiyo mpaka leo nikikumbuka nacheka sana,” aliongeza.

Jambo la pili sitosahau ilikua ni Escape One nilikuwa na shoo baada ya kumaliza nilifuatwa na mama mmoja na watoto zake wa kike akaniambia kuwa ametoka nyumbani na watoto wake wapige nami picha sababu wananipenda sana.

“Nilishangaa sana sababu kwanza hadi mzazi kukubali kuwaleta watoto zake tena wa kike sababu sisi wasanii tunachukuliwa kama wahuni akakubali kuwaleta kwangu ilikuwa ni heshima kubwa sana na siwezi kusahau kabisa,” alisema mwanamuziki huyo.

Country Boy kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Turn Up aliomshirikisha Mwana Fa ambapo mpaka sasa katika mtandao wa Youtube imekwisha tazamwa na watu zaidi ya laki mbili ambapo anakiri kuendeleza kuja zaidi na staili ya muziki tofauti kila siku.

“Zamani nilikua na rap sana ila kwa Turn Up umeona kwa jinsi nilivyobadirika na watu wategemee staili nyingi zaidi hata ya hii waliyoiskia katika Turn Up.”