Khan amuacha mkewe kwa Twitter

Muktasari:

  • Bondia huyo anasubuliwa na tatizo la wivu wa mapenzi

London, England.BONDIA, AMIR Khan ameachana na mkewe, Faryal Makhdoom kupitia ukurasa wake wa Twitter huku akimtuhumu kutoka kimapenzi na bondia, Anthony Joshua.

Lakini, dakika chache mrembo Faryal akaipokea talaka hiyo kwa kujibu kupitia ukurasa wake wa Twitter na baada ya hapo maneno ya shombo yakaanza kwa pande zote kushambuliana.

Kwa sasa wanasubiri uamuzi wa talaka yao mahakamani, lakini wakati Faryal akionekana kusahau na kuendelea na maisha yake, ghafla Khan kaibuka na maneno ya shombo katika kile kinachoonekana bado anamzimia mrembo huyo.

Khan bado anaonekana kumpenda mkewe huyo ambaye kwa sasa ana ujauzito wa bondia huyo na tayari wana mtoto mmoja, Lamaisah.

Imeelezwa kuwa, Khan amekuwa akipuuzia kuweka msisitizo wa talaka hiyo ili kujaribu kunusuru ndoa yake na kumlea mwanaye huyo, lakini Faryal amegoma huku akisisitiza kuwa, chanzo cha mgogoro wao ni familia ya Khan.