Biashara Utd yasajili wapya kumi

Musoma. Biashara United imewatambulisha wachezaji wanne ikiwa ni mwendelezo wao kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Waliotangazwa ni Frank Sekule kutoka Dodoma FC, Lambere Jerome (Lipuli), Daniel Manyenye (Toto Africans) na Yohana Morris mchezaji huru.
Meneja wa timu hiyo, Aman Josiah amesema usajili huo unafikisha wachezaji 10, waliosajiliwa na timu hiyo hadi sasa.
"Usajili huu ni kutokana na mahitaji ya Benchi la Ufundi na kwamba wanaamini nyota hao watafanya vizuri" alisema Josiah.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya timu hiyo, Marwa Mathayo amesema baada ya usajili huo kwa sasa wamebakiza nafasi tatu tu kufunga rasmi zoezi hilo.
"Kamati imejitahidi kusajili nyota bora kutokana na mapendekezo ya makocha, niseme kwamba tumebakiza wachezaji watatu tu ili tufunge rasmi usajili," alisema Mathayo.