Bao la Schulz lampoteza Ozil Ujerumani

Muktasari:

  • Schulz kiungo wa timu ya Hoffenheim ameitwa kwa mara ya kwanza akionekana ndiye amechukua nafasi ya Mesut Ozil aliyestaafu kuitumikia timu hiyo baada ya kutia aibu katika Kombe la Dunia 2018.

Munich, Ujerumani. Bao lililofungwa na mchezaji mpya katika kikosi cha Ujerumani, Nico Schulz limeipa timu hiyo ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Peru.

Schulz kiungo wa timu ya Hoffenheim ameitwa kwa mara ya kwanza akionekana ndiye amechukua nafasi ya Mesut Ozil aliyestaafu kuitumikia timu hiyo baada ya kutia aibu katika Kombe la Dunia 2018.

Kiungo huyo alifunga bao hilo zikiwa zimesalia dakika tano mchezo huo wa kirafiki kumalizika na kumfanya Kocha Joachim Löw, asijutie uamuzi wake wa kumuita.

Ujerumani iliyokuwa bingwa mtetezi wa Kombe la Dunia, haikufanya vizuri katika mechi za kufuzu na pia katika fainali zenyewe zilizofanyika nchini Russia, iliendelea kuboronga na kuwa bingwa wa kwanza kung’olewa hatua ya makundi kwa zaidi ya nusu karne.

Kung’olewa kwa bingwa mtetezi wa Kombe la Dunia katika hatua ya makundi ni tukio ambalo halijawahi kutokea katika kipindi cha miaka 80 iliyopita.

Mchezaji huyo alikuwa kati ya mabadiliko matano ambayo Kocha Low aliyafanya kwenye kikosi chake baada ya mecdhi iliyopita kulazimishwa sare ya bila mabao na Ufaransa Alhamisi iliyopita katika mchezo wa Uefa Nations League.