Amissi Tambwe angekuwepo mngekoma rundo la mabao!

Monday September 11 2017

 

By Gift Macha

Njombe. Benchi la ufundi la Yanga limegundua changamoto mpya katika safu ya ushambuliaji na limepanga kufanya kazi kuhakikisha mambo yanakuwa mazuri.

Yanga ilipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Njombe mji jambo ambalo limewapa hali ya kujiamini kuelekea mchezo ujao dhidi ya Majimaji.

Kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa alisema safu yao ya ushambuliaji ina changamoto kadhaa lakini watazifanyia kazi kabla ya mchezo huo dhidi ya Majimaji.

"Ni kweli tunafunga mabao machache lakini hii imetokana na baadhi ya wachezaji wetu kama Amissi Tambwe. Changamoto nyingine tutazifanyia kazi kabla ya kucheza na Majimaji," alisema Nsajigwa.