Ali Kiba kualiamsha dude kali kuliko Seduce Me

Muktasari:

 

"Oktoba 15 nitaachia ngoma mpya endapo lakini Seduce Me itafikisha watazamaji milioni 10 ndani ya kipindi hiki."

Wakati ngoma yake ya "Seduce Me" ikiendelea kukimbiza ambapo mpaka sasa imeweza kufikisha watazamaji zaidi ya milioni 5, Ali Kiba amepanga kuja na dude lipya si muda tena.

"Oktoba 15 nitaachia ngoma mpya endapo lakini Seduce Me itafikisha watazamaji milioni 10 ndani ya kipindi hiki."

"Hivyo mashabiki wangu wafanye juhudi ili niwaletee picha lenyewe, maana hii ilikuwa trela tu," aliongeza.

Aidha Ali Kiba alifafanua juu ya ishu inayoendelea mitandaoni ambao wanasema kuwa wimbo huo amekopi na si wake.

"Kitu kizuri siku zote, kinapigwa mawe mimi nasema mafanikio ya Seduce Me ni kutokana na ubora wa wimbo na hakuna blah blah hapa," aliongeza.