Ajib afukuzana na Okwi kuweka rekodi

Muktasari:

Yanga inashuka leo uwanjani kutoana jasho na Stand United mjini Shinyanga.

Nyota wa Yanga, Ibrahim Ajib anarejea uwanjani wikiendi hii akiwa na rekodi matata inayotaka kufanana na Emmanuel Okwi.
Ajib ambaye alijiunga na Yanga msimu huu akitokea kwa watani zao Simba, amekuwa na rekodi ya kipekee kwani katika kila mechi aliyofunga Yanga iliondoka na ushindi.
Nyota huyo aliyewahi kuichezea pia Mwadui FC kwa mkopo, amefunga katika michezo dhidi ya Njombe Mji, Lipuli na Kagera Sugar na kuisaidia timu yake kuondoka na alama tisa.
Kwa upande wa Okwi, timu yake imeshinda mara tatu katika mechi nne alizofunga msimu huu. Simba ilishinda dhidi ya Mwadui, Ruvu Shooting na Njombe Mji huku ikipata sare na Mtibwa Sugar, michezo ambayo Okwi alifunga.