ANGALIA VIDEO: Kilichomkuta Manara wakati Okwi akikosa penalti, awajibu Yanga

Timu ya Simba imevurugiwa rekodi yake ambayo walipanga waiweke msimu huu kwa kumaliza mechi zote za Ligi Kuu bila kufungwa, lakini hilo limekwama baada ya Kagera Sugar kuifunga bao 1-0 jana Jumamosi.

Kufungwa kwa Simba limechukuliwa na mashabiki wa Yanga kama kitendo cha fedheha kwa timu hiyo ambayo ilikuwa inakabidhiwa kombe la ubingwa na Rais John Magufuli.

Baada ya Simba kukabidhiwa taji la ubingwa, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Simba, Haji Manara alisema kipigo hicho hakina maana yoyote kwao.
Manara alieleza hayo kwa kusema kuwa lengo kubwa ilikuwa ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara, lakini suala la kufungwa jana wala halileti hasara yoyote kwa sababu tayari wameshachukua ubingwa msimu huu.
Mechezo unaofuata, Simba itakutana na Majimaji FC kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.