21 wachukua fomu Simba

Muktasari:

  • Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Simba, Boniface Lyamwike amesema katika wagombea hao waliochukua fomu, wawili ni wa nafasi ya uenyekiti wakati 19 ni wa nafasi ya ujumbe.

Jumla ya wagombea 21 wamechukua fomu za kuwania uongozi wa nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo utakaofanyika Novemba 3.
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Simba, Boniface Lyamwike amesema katika wagombea hao waliochukua fomu, wawili ni wa nafasi ya uenyekiti wakati 19 ni wa nafasi ya ujumbe.
"Wagombea wawili waliochukua fomu za kuwania nafasi ya uenyekiti ni Mtemi Ramadhani na Swedi Nkwabi lakini pia katika nafasi ya ujumbe, miongoni mwa waliochukua fomu ni akina mama (wanawake) wawili," alisema Lyamwike.
Ingawa hakutaja majina ya waliochukua fomu za kuwania ujumbe, baadhi y vigogo waliochukua fomu ni pamoja na Iddi Kajuna na Mwina Kaduguda wanaowania nafasi za ujumbe wa Bodi ya Simba.
Katika hali ya kushangaza, Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again' amejiweka kando kuwania nafasi yoyote ya uongozi kwenye uchaguzi huo.