Hiki ndicho walichokifanya Simba Ukawa

Katibu wa tawi la Simba Ukawa Hasara Mbalike alisema kwa upande wao msimu huu hawajajaliwa kufanya mambo makubwa lakini wamejipanga kupeleka kikundi cha ushangiliaji kilicho kamili siku ya mechi.

Mbalike alisema wao walikutana kama kikundi na kufanya vikao vizito kuhakikisha msimu unaoanza wanakwenda mahala popote Simba ambapo itakuwa inacheza mechi ili kuwashangilia mwanzo mwisho bila kujali motokeo yoyote ya uwanjani.

"Hatuna tofauti na uongozi wala yoyote ambaye anahusika na Simba hatuna makubwa ya kufanya katika msimu huu ila Simba itakapokuwa na sisi tutakuwepo kuishangilia na kila tunapopata nafasi tutaongea na wachezaji wajitume ili kushinda mechi na kutupa raha ya kushangilia zaidi," alisema Mbalike.