Everton yaifanyizia Manchester United

London, England. Everton imekubali kutoa Pauni 28 milioni kupata saini ya beki wa kati wa Barcelona Yerry Mina.

Mina alikuwa kwenye rada ya Manchester United, lakini ilishindwa kumng’oa kabla ya Everton kuipiku.

Beki huyo wa kimataifa wa Colombia mwenye miaka 23, anakwenda makao makuu Goodison Park kuungana na mchezaji mwenzake wa zamani Barcelona, Lucas Digne.

Mina anaondoka Barcelona baada ya kukosa namba ya kudumu akiwa amecheza mechi sita tangu alipojiunga na klabu hiyo Januari.

Beki huyo aliyeng’ara katika Fainali za Kombe la Dunia, anakuwa mchezaji wa nne kutua Everton akitanguliwa na Richarlison, Joao Virginia na Digne.

Mina hakuwa chaguo la kwanza Barcelona na nafasi kubwa ilichezwa na Samuel Umtiti na Gerard Pique wanaocheza pacha katika kikosi hicho.

Msimu uliopita mchezaji huyo hakutoa mchango licha ya Barcelona kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Hispania na Kombe la Mfalme.

Kocha wa Everton Marco Silva, amevutiwa na kiwango cha Mina akicheza kwa ustadi Fainali za Kombe la Dunia.

Everton itaanza Ligi Kuu England ugenini kuvaana na timu iliyopanda Ligi Kuu Wolverhampton Wanderers kabla ya kuikaribisha Southampton ‘Watakatifu