Australia. Kocha mpya wa Chelsea, Maurizio Sarri akiwa na nyota wake Alvaro Morata na wengine wametua salama Australia na kupata mapokezi makubwa.

Chelsea itacheza mechi yake ya kwanza kirafiki Australia Julai 23 dhidi ya Perth. 

Kocha huyo mpya Maurizio Sarri katika ziara hiyo alikuwa na nyota wake wengi wa kikosi cha kwanza. 

Mashabiki wengi wa Chelsea walijitokeza kuwapokea wachezaji wao na kupiga nao picha kabla ya kuingia kwenye basi.

David Luiz alionekana akisaini picha na jezi za mashabiki hao wakati Marcos Alonso alikuwa akipiga selfie na mashabiki wengi. 

Perth Glory ni timu pekee itakayocheza na Chelsea nchini Australia kabla ya kurejea Ulaya kwa ajili ya kucheza na Inter Milan jijini Nice, Arsenal mjini Dublin na Lyon kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.