Barcelona, Man City zaingia vitani Ulaya

Turin, Italia. Klabu ya Barcelona ya Hispania, imejitosa kuwania saini ya kiungo mahiri wa Juventus ‘Kibibi Kizee’ cha Turin, Miralem Pjanic raia wa Bosnia na Herzegovina.
Barcelona imeibua vita ya aina yake katika kuwania saini ya mchezaji huyo ambaye alianza mazungumzo na mabingwa wa Ligi Kuu England, Man City.
Juventus imeridhia kumuuza mchezaji huyo muda mfupi baada ya kutoa Pauni 105 milioni kumsajili Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid.
“Juventus inataka kuwauza baadhi ya wachezaji ili kukamilisha fedha za kumnunua Ronaldo kwa kuhofia kanuni za fedha za usajili za Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa),” ilisema taarifa ya klabu.
Kocha wa Man City, Pep Guardiola, ameweka bayana nia ya kumsajili Pjanic ambaye ni kiungo bora Juventus.