Harmonize kumtoa Miss Kilimanjaro

Arusha. Mwanamuziki wa kundi la WCB, Harmonize atakonga nyoyo za mashabiki watakaojitokeza kushudia shindano la Miss Kilimanjaro litakalofanyika Jumamosi Julai 14 kwenye ukumbi wa Kili home mkoa wa Kilimanjaro.

 Mkurugenzi wa kampuni ya Dees Bridal Entertainment wandaaji wa shindano hilo Dotto Olafsen amesema jumla ya warembo 15 kutoka viunga mbalimbali vya mkoa huo watachuana kuwania taji la Miss Kilimanjaro.

 Alisema maandalizi ya mashindano hayo yamekamilika kilichobaki ni warembo waonyeshe uwezo wao katika jukwaa kuwania nafasi ya tatu za juu kuwakilisha mkoa katika michuano ya kanda.

"Mwaka huu kauli mbiu yetu ni elimu bure, pedi bure, elimu na haki elimu ili kutokomeza mimba za utotoni na warembo hawa watakuwa mabalozi wa kauli mbiu hii mpaka mwakani tutakapokuwa tunaandaa mashindano mengine," alisema Olafsen.

 Olafsen warembo hao wakiwa kambini wameweza kutafutiwa wataalam wa fani na taaluma mbalimbali ambao walikuwa wanawafundisha kuhusiana na stadi za maisha.

 “Shindano la mwaka huu litakuwa na changamoto kubwa kwa maana warembo wote wameonyesha uwezo wa hali ya juu, na tumeshapanga kiingilio V.I.P A Sh 50,000, VIP B Sh20,000 na viti vya kawaida ni 10,000”