Mbio za Rock City Marathon kutikisa Kirumba

Mwanza. Mbio za Rock City Marathon 2018 zimezinduliwa rasmi jana Jumamosi, ambapo zinatarajia kufanyika Oktoba 28 katika viwanja vya CCM Kirumba jijini hapa.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo,Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya mbio hizo, Zenno Ngowi amesema kuwa wameamua kutangaza mapema ili kutoa muda kwa washiriki kujiandaa vyema.
Amesema kuwa kwa mwaka wa tisa sasa mfululizo wamefanikisha kutoa elimu kuhusu fursa za kitalii na kutangaza vivutio vya utalii kwa Ukanda wa Ziwa Viktoria.
"Leo tunazindua rasmi Mbio za Rock City Marathon kwa mwaka wa tisa mfululizo,lakini mbio hizi zinatarajia kufanyika Oktoba 28 katika viwanja vya CCM Kirumba Mwanza" amesema Ngowi.

Kwa upande Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mery Tesha akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela amesema kuwa wadau wa Utalii na Michezo Kanda ya Ziwa wanapaswa kutumia vyema fursa hiyo kutangaza vivutio vilivyopo katika Mikoa hiyo.
"Woto wangu kwa wadau wa Utalii na Michezo nchini haswa Kanda ya Ziwa, kutumia mbio hizi kutangaza vivutio vya utalii," amesema Mongella.