Simba na Yanga zatishia amani Morogoro

Muktasari:

Na kutokana na hali hiyo, kila mmoja ameweka kuanzia hotelini wanakolala na uwanjani wanakofanya mazoezi yao ambapo Yanga wao waliwawahi Simba na kuulipia mapema Uwanja wa Highland unaoaminika kuwa mzuri zaidi mkoani humo na Msimbazi wakaamua kukimbilia Jamhuri.

KAMBI ya timu za Simba na Yanga huko Morogoro ni moto unaambiwa kwani kila moja imehakikisha mpinzani wake hanasi kitu chochote licha ya kuwa mkoa mmoja na kuimarisha ulinzi ili atakayekosea tu apigike katika mchezo wao wa Aprili 29 utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Simba na Yanga ni watani wa jadi, watakutana katika mchezo huo ambao ndio wanaufanyia maandalizi na safari hii, wamewashangaza wadau wa soka na wale wengine kwa namna walivyoamua kukimbilia Morogoro wote kwa pamoja.

Na kutokana na hali hiyo, kila mmoja ameweka kuanzia hotelini wanakolala na uwanjani wanakofanya mazoezi yao ambapo Yanga wao waliwawahi Simba na kuulipia mapema Uwanja wa Highland unaoaminika kuwa mzuri zaidi mkoani humo na Msimbazi wakaamua kukimbilia Jamhuri.

Kwenye mazoezi yao hayo, makomandoo wao wamehakikisha hakuna mtu mwingine anakwenda kuangalia na anayebahatika kuingia anakuwa amefanya kazi ya maana.