Ndoo ya Morocco, Msuva inamhusu

Muktasari:

Kabla ya mechi yao ya jana usiku dhidi ya vibonde wanaoburuza mkia kwenye msimamo, Racing de Casablanca, Msuva alisema wana kazi kubwa ya kufanya ili kutwaa ubingwa wa Batola Pro.

LIGI Kuu Morocco ‘Batola Pro’ anayocheza mshambuliaji Saimon Msuva, imefika patamu kwa kusaliwa na michezo sita kabla ya mechi za jana (Jumapili) kuamua nani atatwaa ubingwa wa ligi hiyo.

Kabla ya mechi yao ya jana usiku dhidi ya vibonde wanaoburuza mkia kwenye msimamo, Racing de Casablanca, Msuva alisema wana kazi kubwa ya kufanya ili kutwaa ubingwa wa Batola Pro.

“Vigogo ambao tutakutana nao katika mechi zetu zilizosalia ni dhidi ya Raja Casablanca, Olympic Safi, Hassania Agadir na Ittihad Tanger nyingine ni timu za kawaida,” alisema Msuva.

Kama Difaa itawafunga vigogo hao ambao wanawania nao ubingwa huo, watakuwa kwenye mazingira mazuri ya kutwaa ubingwa wa ligi hiyo ambayo walimaliza msimu uliopita kwenye nafasi ya pili.

Difaa ipo nafasi ya tatu wakiwa wamejikusanyia pointi 36, nyuma ya vinara wa ligi hiyo, Ittihad Tanger wenye pointi 44 huku wakifuatiwa na Hassania Agadir pointi 40.