Azam waichapa Jamhuri mabao 4-0

MABINGWA  watetezi wa Kombe la Mapinduzi klabu ya Azam FC,  imeendeleza ubabe katika

michuano hiyo baada ya kuifunga Jamhuri ya Pemba mabao 4-0, katika mchezo uliopigwa Uwanja wa

Amaan, Zanzibar.

Azam walifunga mabao yao dakika ya 16 kupitia kwa straika Mghana Bernald Arthur aliyepokea

krosi ya  Bruce Kangwa.

Kipindi cha pili kilipoanza dakika ya pili,  Salmin Hoza aliifungia Azam bao la pili kwa shuti lililokwenda

moja kwa moja nyavuni, pasi ikitoka kwa Yahya Zaiid.

Zaiid naye aliibuka na kufunga bao la tatu dakika ya 54  kutokana na mpira wa adhabu na wakamaliza kalamu ya mabao yao dakika 79 kupitia kwa Paul Peter .

Hata hivyo, Jamhuri walipata pigo kipindi cha kwanza dakika ya 43 baada ya beki wao, Abdul

Mahafudh kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kumchezea vibaya kiungo wa Azam Joseph Mahundi,

Huo ni mchezo wa pili wa Azam katika mashindano hayo ambapo mchezo wa kwanza, waliifunga

Mwenge ya Pemba mabao 2-0.