Messi kumbe bado hajasaini mkataba!

Muktasari:

  • Raia huyo wa Argentina alikuwa walishakubaliana na uongozi wa Barcelona lakini kuna mambo kadhaa yalitakiwa kufanyiwa marekebisho.

Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi anatarajiwa kusaini mkataba mpya baada ya makubaliano yaliyoafikiwa kufanyiwa marekebisho.

Raia huyo wa Argentina alikuwa walishakubaliana na uongozi wa Barcelona lakini kuna mambo kadhaa yalitakiwa kufanyiwa marekebisho.

Mshambuliaji mwenzake, Luis Suarez anatarajiwa kuwa nje yauwanja kwa mwezi mmoja kutokana na kupata majeraha jambo linalomfanya Messi kuongoza jahazi klabuni hapo.