Kluivert aishangaa PSG kumzuia Verratti kwenda kuichezea Barcelona

Mchezaji wa zamani Patrick Kluivert 

Muktasari:

Verratti amekuwa akihusishwa kujiunga na Barcelona tangu msimu wa 2016/17 lakini klabu yake haina mpango wa kumuuza.

Hispania. Mchezaji wa zamani Patrick Kluivert ameshangazwa na uongozi wa PSG kutoonyesha ni ya kumuachia Marco Verratti anayetaka kwenda kuichezea klabu ya Barcelona.

Verratti amekuwa akihusishwa kujiunga na Barcelona tangu msimu wa 2016/17 lakini klabu yake haina mpango wa kumuuza.

Verratti ana mkataba hadi mwaka 2021 hata hivyo mchezaji huyo amekukosa furaha klabuni hapo baada ya kulikosa taji la ubingwa wa Ligue 1 lililonyakuliwa na Monaco.

Kluivert aliyeitumikia PSG nafasi ya Mkurugenzi wa Soka, mwanzoni mwa mwezi Juni aliachana na majukumu hayo. Hivyo alisema anapenda kuona mchezaji huyo akitua dimba la Camo Nou.

“Namfahamu rais wa klabu vizuri. Verratti aliongezewa mkataba wa miaka minne mwaka jana natambua kwamba Verratti anataka kucheza Barca lakini PSG wanamzuia,” alisema mshambuliaji huyo wa zamani wa Uholanzi.