VIDEO: #WC2018: Pobga awatoa hofu mashabiki fainali Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Aliongeza kuwa bila kudanganya walipoifunga Ujerumani walifikiri ile ndio ilikuwa fanali kwao.
  • Alisema wachezaji walikuwa na uhakika kwamba lazima wataifunga Ureno kwenye fainali hiyo.

Mshambulaji wa Ufaransa, Paul Pogba amejitokeza mble ya waandishi wa  kuwapa somo walilopata baada ya kupoteza mchezo wa fainali Euro 2016 dhidi ya Ureno, wakifungwa bao 1-0.

Pogba alisema wakati wa fainali ya Euro walijua tayari wameshatwaa taji hilo.


Aliongeza kuwa bila kudanganya walipoifunga Ujerumani walifikiri ile ndio ilikuwa fanali kwao.
Alisema wachezaji walikuwa na uhakika kwamba lazima wataifunga Ureno kwenye fainali hiyo.


Aliongeza kuwa hilo ndio lilikiwa kosa kubwa walilofanya. Hata hivyo Pogba alisisitiza kwamba watakuwa makini jambo hilo lisijirudie na wamejiwekea malengo kadhaa.


Nyota huyo, aliahidi kikosi hicho kurekebisha makosa yaliyopita na kusema kwamba mchezo huu mambo yatakuwa tofauti na kuhakikisha kombe linakwenda Ufaransa.