Rapa wa FM Academia aliyezushiwa kifo akata mitaa Mwananyamala

Wednesday June 13 2018

 

By Rhobi Chacha

Rapa anayeitumikia Bendi ya FM Academia anayejulikana Hitler Norma Benga ‘Hitler’ amezushiwa kifo, hata hivyo kiongozi msaidizi wa bendi hyo amethibitisha msanii huyo yupo hai.
Leo asubuhi taarifa zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, radio na televisheshi zikidai kuwa  Hilter amefariki kwa ajali ya pikipiki Kibaha mkoani Pwani.
Hitler ameweka wazi kwamba yupo hai na ameshangaa kuzushiwa habari za kifo ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Aliongeza kuwa baada ya kutokea kwa ajali, mwendesha bodaboda alifariki papo hapo, lakini alipotelewa na simu yake. Hivyo akaamua kurudi nyumbani.
Amesema alishangazwa kusikia watu wakizungumzia taarifa za kifo chake baada ya marafiki zake kukusanyika nyumbani kwake Mwananyamala Kwa Kopa jijini Dar es Salaam
Pia kiongozi Msaidizi wa Bendi ya FM Academia, Christian Mene, amezingumza na Mwanaspoti na kusema kuwa Hilter ni mzima na wala hahusiki na ajali hiyo.
“Kwanza tunawapa pole ndugu zetu wote waliopata usumbufu wa taarifa hizi za Hitler kuwa amefariki. Ukweli ni kwamba hajafariki dunia.”