Picha ya beki Giorgio Chiellini yaibua utata

Friday April 13 2018

 

MADRID HISPANIA


PICHA ya beki wa kati wa Juventus, Giorgio Chiellini imenaswa na kuonyesha kuna kitu kinaitwa kupanga matokeo kilihusika kwenye mechi ya timu yake dhidi ya Real Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya huko Bernabeu juzi Jumatano.

Juve ilitupwa nje ya michuano hiyo baada ya mkwaju wa penalti ya dakika za mwisho wa Cristiano Ronaldo, lakini picha ya Chiellioni akionyesha vidole vyake kama vile kuna pesa inatoka kupewa mwamuzi Michael Oliver akiituhumu Real Madrid baada ya uamuzi wa kupigwa kwa penalti hiyo iliyofanya mechi hiyo isiingie dakika za nyongeza baada ya Juventus kuchomoa bao zote tatu ilizokuwa imefungwa kwenye mechi ya awali. Penalti hiyo ilitokana na beki wa Juventus, Mehdi Benatia kumwangusha Lucas Vazquez ndani ya boksi. Vurugu zikatokea na matokeo yake kipa Gianluigi Buffon akatolewa kwa kadi nyekundu.

Chiellini aliendelea kupinga matokeo hayo na kudai marefa wanaongoza kwa kuipendelea Real Madrid.

“Huu ni uporaji mkubwa niliowahi kuushuhudia katika maisha yangu ya soka,” alisema.

“Haishangazi tena, Bayern Munich ilikumbana na hilo mwaka jana na mwaka huu zamu ya Juve. Imekuwa kawaida Real Madrid kuwa na faida Ligi ya Mabingwa Ulaya.”