Zidane apagawa na Kane

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo wa England amekuwa na msimu mzuri akiwa amefunga mabao sita hadi sasa katika Ligi Kuu England

Zikiwa zimebaki saa chache kabla ya Real Madrid na Tottenham Hotsputrs kuvaana katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, kocha Zinedine Zidane  amemtaja mshambuliaji Harry Kane kuwa bonge la mshambuliaji.

Zidane amekuwa na mapenzi makubwa na mshambuliaji huyo wa Spurs na tayari ameweka bayana anataka kumpa mkataba Santiago Bernabeu.

Kocha huyo wa Real Madrid alisema Kane ni mshambuliaji aliyekamilika na ana sifa zote za kucheza Real Madrid.

Huenda kauli ya nguli huyo wa zamani wa Ufaransa ikamtoa mchezoni Kane ambaye ameonyesha nia ya kutaka kuondoka Makao Makuu White Hart Lane endapo atapewa 'mzigo' wa maana.

Nahodha huyo wa England anatarajia kung'ara katika mchezo huo kwa kuwa yuko katika kiwango bora msimu huu.

"Sijui nini kitatokea baadaye, lakini kwasasa ni mchezaji mahiri aliyekamilika ana kila kitu," alisema Zidane.

Kivutio kingine katika mchezo huo ni kiungo mkabaji wa aina yake Luka Modric ambaye awakarinisha ndugu zake Spurs.

Modric aliwahi kung'ara Spurs kabla ya kutimkia Real Madrid ambapo amekuwa mchezaji nyota wa kiungo duniani.