Kagera Sugar yagawa dozi, yaifuata Biashara Utd

Muktasari:

  • Pamba imeutumia mchezo huo kujiandaa na Ligi Daraja la kwanza inayotarajia kuanza Septemba 29, Kagera wao wanajiandaa dhidi ya Biashara utakaopigwa Jumamosi mjini Musoma mkoani Mara.

Mwanza. Kagera Sugar imeitumia salamu Biashara United baada ya kuibamiza Pamba mabao 4-3 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa jana Jumatano kwenye Uwanja wa Nyamagana jijini hapa.

Pamba imeutumia mchezo huo kujiandaa na Ligi Daraja la kwanza inayotarajia kuanza Septemba 29, Kagera wao wanajiandaa dhidi ya Biashara utakaopigwa Jumamosi mjini Musoma mkoani Mara.

Mabao ya mshambuliaji Christopher Edward 'Edo' aliyeweka mawili kambani dakika ya 3 na 37, Juma Shemvuni dakika ya 33 na Omary Dasashenko dakika ya 44 yalitosha kulaza na maumivu wapinzani wao.

Pamba wao walijipatia mabao yao kupitia kwa Geofrey Julius dakika ya 40, Kelvin John dakika ya 58 na Frank Kilewa dakika ya 67.