KRC Genk ya Samatta yafanya kweli

Muktasari:

  • KRC Genk imevuna pointi zake tatu kwa mara pili kwa kuifunga Anderlecht mabao 2-1 huku nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta akianzia benchi kwenye mchezo huo ambao walikuwa nyumbani, Luminus Arena.

KLABU ya Mbwana Samatta, KRC Genk imeibuka na ushindi wa pili kwenye mchujo (Play Offs1) wa kuwania Ubingwa wa Ligi Kuu Ubelgiji na kushiriki mashindano ya Uefa na Europa league msimu ujao.

KRC Genk imevuna pointi zake tatu kwa mara pili kwa kuifunga Anderlecht mabao 2-1 huku nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta akianzia benchi kwenye mchezo huo ambao walikuwa nyumbani, Luminus Arena.

Mchezo wa kwanza kushinda kwa timu hiyo anayoichezea Mbwana Samatta ulikuwa dhidi ya Standard Liege kwa bao 1-0 baada ya kufungwa dhidi ya Club Brugge KV kwa bao 1-0.

Samatta aliingia kwenye mchezo huo wa pili kwao kushinda dakika ya 83 wakati KRC Genk ikiwa mbele kwa mabao 2-1 na kuchukua nafasi ya Karelis Nikolaos.

Hadi sasa, KRC Genk imemaliza michezo yake mitano ya duru la kwanza la mchujo kwenye duru la pili, itacheza tena na Club Brugge KV, Aprili 27.