Duh! Wenger anawaogopa Arsenal

Tuesday May 15 2018

 

LONDON, ENGLAND

ARSENE Wenger amesema hafikirii kuwa kocha wa timu nyingine ya Ligi Kuu England kwa sababu hajawahi kujiandaa kukabiliana na Arsenal akiwa na timu tofauti.

Juzi Jumapili Wenger aliiongoza Arsenal kwenye mechi yake ya mwisho baada ya kutangaza ataachana na timu hiyo baada ya msimu huu kumalizika na timu yake ilishinda bao 1-0 dhidi ya Huddersfield.