Barcelona yamtengea Coutinho Pauni 80 milioni kumng’oa Liverpool

Muktasari:

  • Barcelona imefikia uamuzi huo baada ya Liverpool kuweka uzibe kwa kumfunga mchezaji huyo kwa dau la Pauni 72 milioni kwa klabu yoyote itakayohitaji huduma yake.

 Klabu ya Barcelona imekoleza moto katika mpango wake wa kumsajili nyota wa Liverpool baada ya kutangaza dau nono la Pauni 80 milioni.

Barcelona imefikia uamuzi huo baada ya Liverpool kuweka uzibe kwa kumfunga mchezaji huyo kwa dau la Pauni 72 milioni kwa klabu yoyote itakayohitaji huduma yake.

Awali, Kocha wa Liverpool alitangaza kwamba mchezaji huyo hauzwi klabuni hapo. Hata hivyo Barcelona wanaonekana hawajakata tamaa dhidi ya kauli  ya kocha huyo hivyo na wamekuja na gia nyingine.